Rukia maudhui
Zaburi 37:7-11

Tulia Katika Bwana na Usubiri kwa Subira

Zaburi 37:7-11
7
Tulia mbele za Bwana na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.
8
Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.
9
Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.
10
Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana, ingawa utawatafuta, hawataonekana.
11
Bali wanyenyekevu watairithi nchi na wafurahie amani tele.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options