Zaburi 37:1-9
1
Zaburi ya Daudi. Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, wala usiwaonee wivu watendao mabaya,
2
kwa maana kama majani watanyauka mara, kama mimea ya kijani watakufa mara.
3
Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.
4
Jifurahishe katika Bwana naye atakupa haja za moyo wako.
5
Mkabidhi Bwana njia yako, mtumaini yeye, naye atatenda hili:
6
Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko, na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.
7
Tulia mbele za Bwana na umngojee kwa uvumilivu; usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, wanapotekeleza mipango yao miovu.
8
Epuka hasira na uache ghadhabu, usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.
9
Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.
Settings