Zaburi 22:12-21
12
Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira.
13
Simba wangurumao wanaorarua mawindo yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.
14
Nimemiminwa kama maji, mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake. Moyo wangu umegeuka kuwa nta, umeyeyuka ndani yangu.
15
Nguvu zangu zimekauka kama kigae, ulimi wangu umegandamana na kaakaa la kinywa changu, kwa sababu umenilaza katika mavumbi ya kifo.
16
Mbwa wamenizunguka, kundi la watu waovu limenizingira, wametoboa mikono yangu na miguu yangu.
17
Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, watu wananikodolea macho na kunisimanga.
18
Wanagawana nguo zangu wao kwa wao, na vazi langu wanalipigia kura.
19
Lakini wewe, Ee Bwana, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie.
20
Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.
21
Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.
Settings