Skip to content
Zaburi 18:20-30

Zaburi 18:20-30

20
Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
21
Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
22
Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.
23
Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi.
24
Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.
25
Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia.
26
Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi.
27
Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini huwashusha wenye kiburi.
28
Wewe, Ee Bwana, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka; Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga.
29
Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta.
30
Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options