Zaburi 148:7-14
7
Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,
8
umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,
9
ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote,
10
wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao,
11
wafalme wa dunia na mataifa yote, ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,
12
wanaume vijana na wanawali, wazee na watoto.
13
Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.
14
Amewainulia watu wake pembe, sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. Msifuni Bwana.
Settings