Skip to content
Zaburi 145:1-9

Zaburi 145:1-9

1
Wimbo wa Sifa. Wa Daudi. Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele.
2
Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.
3
Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
4
Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.
5
Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
6
Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu.
7
Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.
8
Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.
9
Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options