Zaburi 136:1-9
1
Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.
2
Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele.
3
Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele.
4
Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele.
5
Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele.
6
Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele.
7
Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele.
8
Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele.
9
Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele.
Settings