Zaburi 135:5-12
5
Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu, kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.
6
Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote.
7
Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua na huleta upepo kutoka ghala zake.
8
Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama.
9
Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri, dhidi ya Farao na watumishi wake wote.
10
Aliyapiga mataifa mengi, na akaua wafalme wenye nguvu:
11
Mfalme Sihoni na Waamori, Ogu mfalme wa Bashani na wafalme wote wa Kanaani:
12
akatoa nchi yao kuwa urithi, urithi kwa watu wake Israeli.
Settings