Zaburi 135:15-18
15
Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
16
Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, zina macho, lakini haziwezi kuona;
17
zina masikio, lakini haziwezi kusikia, wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.
18
Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
Settings