Zaburi 119:129-136
129
Sheria zako ni za ajabu, hivyo ninazitii.
130
Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru, kunampa mjinga ufahamu.
131
Nimefungua kinywa changu na kuhema, nikitamani amri zako.
132
Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote wale wanaolipenda jina lako.
133
Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako, usiache dhambi yoyote initawale.
134
Niokoe na uonevu wa wanadamu, ili niweze kutii mausia yako.
135
Mwangazie mtumishi wako uso wako na unifundishe amri zako.
136
Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu, kwa kuwa sheria yako haifuatwi.
Settings