Skip to content
Zaburi 109:6-20

Zaburi 109:6-20

6
Agiza mtu mwovu ampinge, mshtaki asimame mkono wake wa kuume.
7
Anapohukumiwa, apatikane na hatia, nayo maombi yake yamhukumu.
8
Siku zake za kuishi na ziwe chache, nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine.
9
Watoto wake na waachwe yatima, mke wake na awe mjane.
10
Watoto wake na watangetange wakiomba, na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao.
11
Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo, matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni.
12
Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema wala wa kuwahurumia yatima wake.
13
Uzao wake na ukatiliwe mbali, majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.
14
Maovu ya baba zake na yakumbukwe mbele za Bwana, dhambi ya mama yake isifutwe kamwe.
15
Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.
16
Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.
17
Alipenda kulaani, nayo laana ikampata; hakupenda kubariki, kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.
18
Alivaa kulaani kama vazi lake, nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji, kwenye mifupa yake kama mafuta.
19
Na iwe kama joho alilozungushiwa, kama mshipi aliofungiwa daima.
20
Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, kwa wale wanaoninenea mabaya.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options