Mithali 9:7
Inaonyesha mstari 7 pamoja na muktadha unaouzunguka.
4
Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa!
5
Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya.
6
Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
7
“Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha hukaribisha matukano; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi.
8
Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda.
9
Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi; mfundishe mtu mwadilifu naye atazidi kufundishika.
10
“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
Settings