Mithali 9:13-18
13
Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele; hana adabu na hana maarifa.
14
Huketi kwenye mlango wa nyumba yake, juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji,
15
akiita wale wapitao karibu, waendao moja kwa moja kwenye njia yao.
16
Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!”
17
“Maji yaliyoibiwa ni matamu; chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!”
18
Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo, kwamba wageni wake huyo mwanamke wako katika vilindi vya kuzimu.
Settings