Mithali 9:1-6
1
Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo zake saba.
2
Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake.
3
Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita kutoka mahali pa juu sana pa mji.
4
Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa!
5
Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya.
6
Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
Settings