Mithali 18:1-5
1
Mtu ajitengaye na wengine hufuata matakwa yake mwenyewe; hupiga vita kila shauri jema.
2
Mpumbavu hafurahii ufahamu, bali hufurahia kutangaza maoni yake mwenyewe.
3
Wakati uovu unapokuja, dharau huja pia, pamoja na aibu huja lawama.
4
Maneno ya kinywa cha mwanadamu ni kina cha maji, bali chemchemi ya hekima ni kijito kinachobubujika.
5
Sio vizuri kumpendelea mtu mwovu, au kumnyima haki asiye na hatia.
Settings