Skip to content
Mathayo 5:38-42

Mathayo 5:38-42

38
“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’
39
Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia.
40
Kama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia.
41
Kama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili.
42
Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options