Mathayo 15:38
Inaonyesha mstari 38 pamoja na muktadha unaouzunguka.
35
Yesu akawaambia ule umati wa watu waketi chini.
36
Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akiisha kumshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa ule umati wa watu.
37
Wote wakala na kushiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba.
38
Idadi ya watu walikuwa wanaume 4,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.
39
Baada ya kuaga ule umati wa watu, Yesu aliingia katika mashua, akaenda sehemu za Magadani.
Settings