Marko 13:24-26
24
“Lakini katika siku hizo, baada ya hiyo dhiki, “ ‘jua litatiwa giza nao mwezi hautatoa nuru yake;
25
nazo nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za anga zitatikisika.’
26
“Ndipo watu wote watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.