Skip to content
Luka 18:32-43

Luka 18:32-43

32
Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa watu wasiomjua Mungu, nao watamdhihaki, watamtukana na kumtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua.
33
Naye siku ya tatu atafufuka.”
34
Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya, kwa kuwa maana yake ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Yesu alikuwa anazungumzia nini.
35
Yesu alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada.
36
Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita, akauliza, “Kuna nini?”
37
Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”
38
Akapaza sauti, akasema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”
39
Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”
40
Yesu akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza,
41
“Unataka nikufanyie nini?” Akajibu, “Bwana, nataka kuona.”
42
Yesu akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.”
43
Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options