Waamuzi 5:23
Inaonyesha mstari 23 pamoja na muktadha unaouzunguka.
20
Kutoka mbinguni nyota zilipigana, nyota kutoka njia zake zilipigana na Sisera.
21
Mto wa Kishoni uliwasomba, ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. Songa mbele, ee nafsi yangu, kwa ujasiri!
22
Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo: farasi wake wenye nguvu huenda mbio kwa kurukaruka.
23
Malaika wa Bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe. Walaaniwe watu wake kwa uchungu, kwa kuwa hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’
24
“Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, mkewe Heberi, Mkeni, abarikiwe kuliko wanawake wote waishio kwenye mahema.
25
Aliomba maji, naye akampa maziwa; kwenye bakuli la heshima akamletea maziwa mgando.
26
Akanyoosha mkono wake akashika kigingi cha hema, mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi. Akampiga Sisera kwa nyundo, akamponda kichwa chake, akamvunjavunja na kumtoboa paji lake la uso.
Settings