Ayubu 4:7-9
7
“Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia? Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa?
8
Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza, wale walimao ubaya na wale hupanda uovu, huvuna hayo hayo hayo.
9
Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa; kwa mshindo wa hasira zake huangamia.