Ayubu 30:24
Inaonyesha mstari 24 pamoja na muktadha unaouzunguka.
21
Wewe unanigeukia bila huruma; unanishambulia kwa nguvu za mkono wako.
22
Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali.
23
Ninajua utanileta mpaka kifoni, mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa.
24
“Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji, anapoomba msaada katika shida yake.
25
Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini?
26
Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.
27
Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili.
Settings