Ayubu 30:20-24
20
“Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu; ninasimama, nawe unanitazama tu.
21
Wewe unanigeukia bila huruma; unanishambulia kwa nguvu za mkono wako.
22
Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali.
23
Ninajua utanileta mpaka kifoni, mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa.
24
“Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji, anapoomba msaada katika shida yake.
Settings