Skip to content
Yeremia 7:1-7

Yeremia 7:1-7

1
Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana:
2
“Simama kwenye lango la nyumba ya Bwana, na huko upige mbiu ya ujumbe huu: “ ‘Sikieni neno la Bwana, enyi watu wote wa Yuda mliokuja kupitia malango haya ili kumwabudu Bwana.
3
Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Tengenezeni njia zenu na matendo yenu, nami nitawaacha mkae mahali hapa.
4
Msitumainie maneno ya udanganyifu na kusema, “Hili ni Hekalu la Bwana, Hekalu la Bwana, Hekalu la Bwana!”
5
Kama kweli mkibadili njia zenu na matendo yenu, mkatendeana haki kila mmoja na mwenzake,
6
kama msipomwonea mgeni, yatima wala mjane, na kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, nanyi kama msipofuata miungu mingine kwa madhara yenu wenyewe,
7
ndipo nitawaacha mkae mahali hapa, katika nchi niliyowapa baba zenu milele na milele.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options