Yeremia 2:29-37
29
“Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu? Ninyi nyote mmeniasi,” asema Bwana.
30
“Nimeadhibu watu wako bure tu, hawakujirekebisha. Upanga wako umewala manabii wako kama simba mwenye njaa.
31
“Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno la Bwana: “Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli au nchi ya giza kuu? Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura, hatutarudi kwako tena’?
32
Je, mwanamwali husahau vito vyake, au bibi arusi mapambo yake ya arusi? Lakini watu wangu wamenisahau mimi, tena kwa siku zisizo na hesabu.
33
Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi! Hata wale wanawake wabaya kuliko wote wanaweza kujifunza kutokana na njia zako.
34
Katika nguo zako watu huona damu ya uhai ya maskini wasio na hatia, ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba. Lakini katika haya yote
35
unasema, ‘Sina hatia; Mungu hajanikasirikia.’ Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema, ‘Mimi sijatenda dhambi.’
36
Kwa nini unatangatanga sana, kubadili njia zako? Utakatishwa tamaa na Misri kama ulivyokatishwa na Ashuru.
37
Pia utaondoka mahali hapo ukiwa umeweka mikono kichwani, kwa kuwa Bwana amewakataa wale unaowatumainia; hutasaidiwa nao.
Settings