Yeremia 2:1-6
1
Neno la Bwana lilinijia kusema,
2
“Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu: “ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako, jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi na kunifuata katika jangwa lile lote, katika nchi isiyopandwa mbegu.
3
Israeli alikuwa mtakatifu kwa Bwana, kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake; wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia, nayo maafa yaliwakumba,’ ” asema Bwana.
4
Sikia neno la Bwana, ee nyumba ya Yakobo, nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli.
5
Hivi ndivyo asemavyo Bwana: “Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu, hata wakatangatanga mbali nami hivyo? Walifuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai.
6
Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’
Maandiko ya Biblia: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)™, © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. · CC BY-SA 4.0“Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc., used with permission.
Settings