Hosea 4:15-19
15
“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli, Yuda naye asije akawa na hatia. “Usiende Gilgali, usipande kwenda Beth-Aveni Wala usiape, ‘Hakika kama Bwana aishivyo!’
16
Waisraeli ni wakaidi, kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi. Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga kama wana-kondoo katika shamba la majani?
17
Efraimu amejiunga na sanamu, ondokana naye!
18
Hata wakati wamemaliza vileo vyao wanaendelea na ukahaba wao, watawala wao hupenda sana njia za aibu.
19
Kisulisuli kitawafagilia mbali na dhabihu zao zitawaletea aibu.
Settings