Waebrania 7:19-21
19
(kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu.
20
Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote,
21
lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia: “Bwana ameapa naye hatabadilisha mawazo yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’ ”
Settings