Mwanzo 49:16-18
16
“Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli.
17
Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, nyoka mwenye sumu kando ya njia, yule aumaye visigino vya farasi ili yule ampandaye aanguke chali.
18
“Ee Bwana, nautafuta wokovu wako.