Skip to content
Mwanzo 49:13-18

Mwanzo 49:13-18

13
“Zabuloni ataishi pwani ya bahari na kuwa bandari za kuegesha meli; mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni.
14
“Isakari ni punda mwenye nguvu ambaye amelala kati ya mizigo yake.
15
Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika na jinsi nchi yake inavyopendeza, atainamisha bega lake kwenye mzigo na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu.
16
“Dani atahukumu watu wake kwa haki kama mmoja wa makabila ya Israeli.
17
Dani atakuwa nyoka kando ya barabara, nyoka mwenye sumu kando ya njia, yule aumaye visigino vya farasi ili yule ampandaye aanguke chali.
18
“Ee Bwana, nautafuta wokovu wako.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options