Mwanzo 38:1-5
1
Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake, akaenda kuishi na Hira Mwadulami.
2
Huko Yuda akakutana na binti wa Kikanaani aitwaye Shua, akamwoa na akakutana naye kimwili,
3
akapata mimba, akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri.
4
Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita Onani.
5
Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita Shela. Huyu alimzalia mahali paitwapo Kezibu.
Settings