Skip to content
Mwanzo 17:23-27

Mwanzo 17:23-27

23
Siku ile ile, Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza.
24
Abrahamu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa,
25
naye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu.
26
Abrahamu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku ile ile,
27
Kila mwanaume nyumbani mwa Abrahamu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options