Rukia maudhui
Ezekieli 45:9-12

Wajibu wa maadili wa mkuu

Ezekieli 45:9-12
9
“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Yatosha, enyi wakuu wa Israeli! Acheni mbali ukatili wenu na uonevu wenu mkafanye lile lililo haki na sawa. Acheni kuwatoza watu wangu isivyo haki, asema Bwana Mwenyezi.
10
Tumieni mizani sahihi na vipimo sahihi vya efa na bathi.
11
Efa na bathi viwe sawa, bathi iwe sehemu ya kumi ya homeri na efa iwe sehemu ya kumi ya homeri, homeri itakuwa ndicho kiwango cha kukubalika kwa vyote viwili.
12
Shekeli moja itakuwa gera ishirini. Shekeli ishirini, jumlisha na shekeli ishirini na tano, jumlisha na shekeli kumi na tano zitakuwa mina moja.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options