Kutoka 22:21-27
21
“Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.
22
“Usimdhulumu mjane wala yatima.
23
Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.
24
Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.
25
“Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba.
26
Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama,
27
kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma.
Settings