Skip to content
Mhubiri 11:1-6

Mhubiri 11:1-6

1
Tupa mkate wako juu ya maji, kwa maana baada ya siku nyingi utaupata tena.
2
Wape sehemu watu saba, naam hata wanane, kwa maana hujui ni baa gani litakalokuwa juu ya nchi.
3
Kama mawingu yamejaa maji, hunyesha mvua juu ya nchi. Kama mti ukianguka kuelekea kusini au kuelekea kaskazini, mahali ulipoangukia, hapo ndipo utakapolala.
4
Yeyote atazamaye upepo hatapanda, yeyote aangaliaye mawingu hatavuna.
5
Kama vile usivyofahamu njia ya upepo, au jinsi mwili uumbwavyo ndani ya tumbo la mama, vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu, Muumba wa vitu vyote.
6
Panda mbegu yako asubuhi, nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee, kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa, kwamba ni hii au ni ile, au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options