Kumbukumbu 27:9-26
9
Kisha Mose na makuhani, ambao ni Walawi, wakawaambia Israeli wote, “Nyamaza ee Israeli, sikiliza! Sasa umekuwa taifa la Bwana Mungu wako.
10
Mtii Bwana Mungu wako, na kufuata amri zake na maagizo ninayokupa leo.”
11
Siku ile ile Mose akawaagiza watu:
12
Mtakapovuka Mto Yordani, makabila haya yatasimama juu ya Mlima Gerizimu kubariki watu: Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Yosefu na Benyamini.
13
Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.
14
Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa:
15
“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.”
16
“Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.”
17
“Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.”
18
“Alaaniwe mtu ampotoshaye kipofu njiani.”
19
“Alaaniwe mtu apotoshaye haki ya mgeni, yatima au mjane.”
20
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mke wa baba yake, kwa maana anadharau malazi ya baba yake.”
21
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.”
22
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na dada yake, binti wa baba yake au binti wa mama yake.”
23
“Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mama mkwe wake.”
24
“Alaaniwe mtu amuuaye jirani yake kwa siri.”
25
“Alaaniwe mtu apokeaye rushwa ili kumuua mtu asiye na hatia.”
26
“Alaaniwe mtu yule ambaye hatashikilia maneno ya sheria hii kwa kuyatekeleza.”
Settings