Skip to content
1 Wakorintho 12:12-20

1 Wakorintho 12:12-20

12
Kama vile mwili ulivyo mmoja nao una viungo vingi, navyo viungo vyote vya mwili ingawa ni vingi, ni mwili mmoja, vivyo hivyo na Kristo.
13
Kwa maana katika Roho mmoja wote tulibatizwa katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wayunani, kama ni watumwa au watu huru, nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
14
Basi mwili si kiungo kimoja, bali ni viungo vingi.
15
Kama mguu ungesema, “Kwa kuwa mimi si mkono basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya huo mguu usiwe sehemu ya mwili.
16
Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si wa mwili,” hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili.
17
Kama mwili wote ungelikuwa jicho, kusikia kungekuwa wapi? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, kunusa kungekuwa wapi?
18
Lakini kama ilivyo, Mungu ameweka viungo katika mwili, kila kimoja kama alivyopenda.
19
Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
20
Kama ulivyo, una viungo vingi, lakini mwili ni mmoja.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options