Skip to content
1 Nyakati 7:13

1 Nyakati 7:13

Inaonyesha mstari 13 pamoja na muktadha unaouzunguka.
10
Mwana wa Yediaeli alikuwa: Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari.
11
Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.
12
Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.
13
Wana wa Naftali walikuwa: Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.
14
Wana wa Manase walikuwa: Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi.
15
Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.
16
Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options