Skip to content
1 Nyakati 5:18-26

1 Nyakati 5:18-26

18
Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa na watu mashujaa 44,760 waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya vita: watu wenye nguvu, hodari wa kutumia ngao na upanga, mashujaa wa kutumia upinde, waliokuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo.
19
Walipigana vita dhidi ya Wahagari, Yeturi, Nafishi na Nodabu.
20
Walisaidiwa katika kupigana nao, Mungu akawatia Wahagari pamoja na wote walioungana nao mikononi mwao, kwa sababu walimlilia Mungu wakati wa vita. Alijibu maombi yao, kwa sababu walimtegemea.
21
Walitwaa mifugo ya Wahagari: ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000. Pia wakateka watu 100,000,
22
na wengine wengi waliuawa kwa sababu vita vilikuwa ni vya Mungu. Nao waliendelea kuikalia nchi hiyo mpaka wakati wa uhamisho.
23
Idadi ya nusu ya kabila la Manase walikuwa wengi sana, Wakakaa kuanzia Bashani hadi Baal-Hermoni, yaani mpaka Seniri na mlima Hermoni.
24
Hawa ndio waliokuwa viongozi wa jamaa za kabila hilo: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia na Yahdieli. Walikuwa askari shujaa watu maarufu, viongozi wa jamaa zao.
25
Lakini hawakuwa waaminifu kwa Mungu wa baba zao, nao wakafanya ukahaba kwa miungu ya mataifa, ambayo Mungu alikuwa ameyaangamiza mbele yao.
26
Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options