Skip to content
1 Nyakati 3:1-9

1 Nyakati 3:1-9

1
Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;
2
wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;
3
wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali; wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.
4
Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita. Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu,
5
nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu: mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua, Shobabu, Nathani na Solomoni.
6
Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti,
7
Noga, Nefegi, Yafia,
8
Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa.
9
Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options