Skip to content
1 Nyakati 3:1-4

Wana wa Daudi waliozaliwa Hebroni

1 Nyakati 3:1-4
1
Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni: Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli; wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;
2
wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;
3
wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali; wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.
4
Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita. Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu,
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options