1 Nyakati 23:6-23
6
Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
7
Wana wa Wagershoni walikuwa wawili: Ladani na Shimei.
8
Wana wa Ladani walikuwa watatu: Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.
9
Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomothi, Hazieli na Harani. Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.
10
Nao wana wa Shimei walikuwa wanne: Yahathi, Zina, Yeushi na Beria.
11
Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.
12
Wana wa Kohathi walikuwa wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
13
Wana wa Amramu walikuwa: Aroni na Mose. Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele za Bwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina la Bwana milele.
14
Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.
15
Wana wa Mose walikuwa: Gershomu na Eliezeri.
16
Wazao wa Gershomu: Shebueli alikuwa wa kwanza.
17
Wazao wa Eliezeri: Rehabia alikuwa wa kwanza. Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
18
Wana wa Ishari: Shelomithi alikuwa wa kwanza.
19
Wana wa Hebroni walikuwa: Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.
20
Wana wa Uzieli walikuwa: Mika wa kwanza na Ishia wa pili.
21
Wana wa Merari walikuwa: Mahli na Mushi. Wana wa Mahli walikuwa: Eleazari na Kishi.
22
Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
23
Wana wa Mushi: Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.
Settings