Skip to content
1 Nyakati 1:43-50

1 Nyakati 1:43-50

43
Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
44
Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
45
Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
46
Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
47
Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
48
Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.
49
Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
50
Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options