Zaburi126
Listen to this chapter
0:00
0:00
Kukumbuka kwa Furaha Kurejeshwa
1
Wimbo wa kwenda juu. Bwana alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto.
2
Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “Bwana amewatendea mambo makuu.”
3
Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha.
Maombi ya Kurejeshwa Kikamilifu na Mavuno
4
Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu.
5
Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe.
6
Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake.
Settings
Reading style
Typeface
Font size px
Reading width chars
Options
Study note