Skip to content
Ruthu 1:1-5

Ruthu 1:1-5

1
Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu.
2
Mtu huyu aliitwa Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa Waefrathi kutoka Bethlehemu ya Yuda. Wakaenda katika nchi ya Moabu, wakaishi huko.
3
Elimeleki mumewe Naomi akafa, hivyo Naomi akabaki na wanawe wawili.
4
Nao wakaoa wanawake Wamoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa, na wa pili aliitwa Ruthu. Baada ya kama miaka kumi,
5
Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options