Warumi 16:1-4
1
Napenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe, mtumishi katika kanisa la Kenkrea.
2
Naomba mpokeeni katika Bwana ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao.
3
Wasalimuni Prisila na Akila, watumishi wenzangu katika Kristo Yesu.
4
Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu; wala si mimi tu ninayewashukuru bali pia makanisa yote ya watu wa Mataifa.
Settings