Zaburi 95:1-7
1
Njooni, tumwimbie Bwana kwa furaha; tumfanyie kelele za shangwe Mwamba wa wokovu wetu.
2
Tuje mbele zake kwa shukrani, tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.
3
Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu, mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4
Mkononi mwake mna vilindi vya dunia, na vilele vya milima ni mali yake.
5
Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu.
6
Njooni, tusujudu, tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Muumba wetu,
7
kwa maana yeye ndiye Mungu wetu, na sisi ni watu wa malisho yake, kondoo chini ya utunzaji wake. Kama mkiisikia sauti yake leo,
Settings