Skip to content
Zaburi 77:13-18

Zaburi 77:13-18

13
Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?
14
Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.
15
Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu.
16
Maji yalikuona, Ee Mungu, maji yalikuona yakakimbia, vilindi vilitetemeka.
17
Mawingu yalimwaga maji, mbingu zikatoa ngurumo kwa radi, mishale yako ikametameta huku na huko.
18
Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli, umeme wako wa radi ukaangaza dunia, nchi ikatetemeka na kutikisika.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options