Zaburi 77:1-2
1
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu. Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie.
2
Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijika.