Zaburi 37:12-15
12
Waovu hula njama dhidi ya wenye haki na kuwasagia meno,
13
bali Bwana huwacheka waovu, kwa sababu anajua siku yao inakuja.
14
Waovu huchomoa upanga na kupinda upinde, ili wawaangushe maskini na wahitaji, kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu.
15
Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe, na pinde zao zitavunjwa.
Settings